"Leo haitakuwa rahisi, lakini tutawapiga kwa style hii" - Gamondi
Eric Buyanza
December 8, 2023
Share :
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema matokeo rafiki kwao leo kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana ni ushindi tu ili kuendelea kuwa kwenye matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano.
"Ni lazima tushinde, tunajua haitakuwa rahisi lakini tutafanya, tuna alama moja tu kati ya 6 tulizopaswa kuvuna, tulifanya makosa na tulihitajika kujifunza kupitia makosa hayo, tumejidhatiti kupata alama 3 dhidi ya Medeama na imani tutazipata" alisema Gamondi kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huu.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiburuza mkia wa kundi D baada ya kuvuna alama moja pekee kwenye michezo miwili ya kundi hilo aambalo mbali na Medeam lina timu kama CR Belouizdad na Al Ahly.