pmbet

Leo ni leo, Azam vs Yanga kwa mkapa, mambo haya kunogesha Vita

Sisti Herman

March 17, 2024
Share :

Mbivu na mbichi leo machi 17 zitajulikana wazi kwenye dimba la Benjamin Mkapa ambapo itachezwa mechi kubwa kwenye ligi kuu Tanzania bara klabu ya Azam itakapowakaribisha Yanga kuanzia saa 2 na nusu usiku.

 

Mambo Matano 5 muhimu kuyajua kwenye vita hii;

 

1. Vita ya msimamo

 

Yanga wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 52 baada ya michezo 19 huku Azam wakiwa nafasi ya 3 na alama zao 44 baada ya michezo 20 na endapo leo watashinda watapanda hadi nafasi ya pili juu ya Simba huku wakiwa na mchezo mmoja zaidi.

 

2. Vita ya rekodi

 

Katika michezo 20 iliyopita kwa timu hizi, Yanga imeshinda mara 10, Azam imeshinda mara 5 na sare 5, huku kwenye michezo minne mfululizo iliyopita baina yao Yanga akiibuka na ushindi mara zote, hivyo mchezo wa leo ni aidha Yanga waendeleze ubabe au Azam waukatae ubabe.

 

3. Vita ya ufungaji

 

Kwenye msimamo wa wanaongoza kwa ufungaji kwenye ligi hiyo hadi sasa Stephanie Aziz Ki wa Yanga anaongoza kwa magoli 13 huku akifuatiwa na Feisal Salum wa Azam mwenye magoli 12.

 

4. Viingilio

 

Viingilio vya mchezo huo kwa mujibu wa klabu mwenyeji wa mchezo ni Shilingi 5,000 mzunguko, 10,000 V.I.P B/C na 20,000 V.I.P A.

 

5. Vita ya mbinu

 

Vita kamili itaamuliwa na mbinu za makocha wawili, Youssouf Dabo wa Azam na Miguel Gamondi wa Yanga ambao kimsingi ndiyo waliobeba mikoba iliyoficha ubora na udhaifu wa pande zote mbili ambayo itaenda kuwasilishwa Benjamin Mkapa na ufundi maridhawa wa wachezaji wa pande zote mbili

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet