Leo ni leo, Chelsea na Liverpool nani Bingwa Carabao Cup?
Sisti Herman
February 25, 2024
Share :
Leo katika dimba la Wembley mida ya saa 12:00 jioni, Chelsea na Liverpool zitakutana hapo kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao ambapo mshindi atapokea zawadi ya Pauni 100,000 ambazo ni sawa na Sh322 milioni za Kitanzania.
Mechi hii ambayo itaanza saa machache kutoka hivi sasa, timu itakayopoteza itapata Pauni dola 50,000 ambazo ni sawa na Sh161 milioni za Kibongo.
Kwa upande wa timu zilizoishia hatua ya nusu fainali, Fulham na Middlesbrough zenyewe zitapata Pauni 25,000 ambazo ni Sh80 milioni kwa pesa ya Tanzania.
Mchezo huu unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni ambapo kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino yeye atakuwa anataka kuondoa gundu kwa kushinda taji lake la kwanza tangu atue Chelsea wakati kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anahitaji kushinda ili kujihakikishia anawaaga mashabiki wa Liverpool na taji baada ya kutangaza kuondoka mwisho wa msimu huu.
Pesa hii ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi ambacho anakipata bingwa wa Ligi Kuu England ambacho kinafikia Pauni 150 milioni huku bingwa wa Kombe la FA hutia kibindoni Pauni 4 milioni.