Leo ni vita ya kurudisha heshima
Eric Buyanza
November 30, 2024
Share :
Namungo na Yanga zinakutana leo Mkoani Lindi kwenye Uwanja wa Majaliwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu, huku timu zote zikiwa hazijapata ushindi kwenye michezo ya karibuni jambo litakaloufanya mchezo huo kuwa mgumu kwani kila kikosi kitakuwa kikitafuta matokeo mazuri ili kurudisha imani kwa mashabiki.
Yanga itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Azam Novemba 2 na Tabora United Novemba 7.
Namungo na Yanga zimekutana mara 10 kwenye Ligi Kuu ambapo Yanga imeshinda michezo 5 na kupata sare 5 huku Namungo ikiwa haijashinda hata mchezo mmoja.