Leroy aitupa Bayern asaini kandarasi ya miaka 3 kuichezea Galatasaray
Eric Buyanza
June 12, 2025
Share :
Leroy Sane ameamua kuondoka Bayern Munich ili kutafuta changamoto mpya huko Galatasaray na tayari ameshasaini kandarasi ya kuichezea klabu hiyo ya Uturuki kwa miaka 3.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa kwenye mazungumzo na mabingwa hao wa Bundesliga kuhusu kandarasi mpya msimu mzima lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa na anaondoka akiwa mchezaji huru.
Bayern ilimpa Sane nyongeza ya kandarasi ya miaka mitatu lakini kwa masharti ya kumpunguzia mshahara, pendekezo ambalo lilikataliwa na Sané.