Levekursen ya Xabi Alonso yamaliza msimu bila kufungwa Bundesliga
Sisti Herman
May 19, 2024
Share :
Baada ya jana kucheza mchezo wao wa mwisho wa Bundesliga na kudhinda 2-1 dhidi ya Augsburg, klabu ya Bayer Levekursen imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza kumaliza msimu kwenye ligi kuu Ujerumani bila kufungwa.
Leverkusen ambao wapo chini ya kocha kijana Xabi Alonso walitawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo mechi 5 kabla msimu haujatamatika jana wameweka historia hiyo baada ya kuicheza michezo 34 wakashinda 28 na kutoa sare 6.
Bado Leverkusen wana nafasi ya kuwa timu ya kwanza kwenye historia kumaliza msimu bila kufungwa kwenye michuano yote kama endapo watashinda michezo yao ya fainali za mashindano waliyonigia ambayo ni kombe la ligi ya Ulaya (Europa League) ambapo watacheza dhidi ya Atlanta ya Italia na kombe la ligi ya Ujerumani (DFB Pokal) ambapo watacheza dhidi ya Kaiserslautern.