Levekursen yamaliza msimu bila kuifungwa Ujerumani
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Klabu ya Bayer Levekursen inayonolewa na kocha kijana Xabi Alonso imeweka Historia rasmi baada ya kumaliza michuano yote nchini ya Ujerumani kwa kutwaa makombe yote makubwa bila kufungwa mechi hata moja.
Levekursen imeweka rekodi hiyo jana baada ya kushinda mchezo wao wa fainali ya kombe la FA ya Ujerumani maarufu kama DFB Pokal kwa kuitandika klabu ya Kaiserslautern ya ligi daraja la kwanza goli 1-0 ambalo limefungwa na nahodha Granit Xhaka.
Levekusern waki iliyopita walibeba taji la Bundesliga kwa kumaliza msimu bila kufungwa, ikiwa timu ya kwanza kuandika historia hiyo kwenye Bundesliga.