Leverkusen wamegoma kufungwa tena
Sisti Herman
April 19, 2024
Share :
Mara baada ya wikiendi iliyopita kutwaa ubingwa Bundesliga huku ikibakiwa na michezo mitano mkononi bila kuruhusu kufungwa hadi sasa, Bayer Lverkusen jana usiku baada ya sare ya 'mbinde' dhidi ya West Ham imefikia rekodi ya kutofungwa michezo mingi kwenye mashindano yote barani Ulaya ilikuwa ikishikiliwa na klabu ya Juventus baada ya kufikisha michezo 44 bila kuruhusu kufungwa mchezo wowote, ikiwa timu pekee Ulaya msimu huu.
Sare hiyo ya 1-1 iliyotokana na bao la jioni la Jerome Frimpong dakika ya 89 ambaye aalisawazisha ubao baada ya West Ham kuongoza kwa zaidi ya dakika 80 kupitia goli la mshambuliaji wao Michael Antonio, inawafanya Lverkusen kusonga hatua ya nusu fainali ya Europa League.
Leverkusen iliyopo chini ya kocha Xabi Alonso itacheza nusu fainali dhidi ya AS Roma.