Leverkusen wameshindikana, waikanda West Ham London
Sisti Herman
April 12, 2024
Share :
Mara baada ya kutofungwa kwenye michezo 41 mfululizo kwenye michuano yote msimu huu, jana klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani iliyopo chini ya kocha kijana Xabi Alonso imefikisha michezo 42 bila kufungwa mbele ya klabu ya West ham ya Uingereza baada ya ushindi wa 2-0 kwenye Europa League jijini London.
Hiyo ni rekodi kubwa sana kwa klabu hiyo kwani hadi sasa haijapoteza mchezo wowote wa ;
- Ligi kuu Ujerumani, raundi ya 28
- Kombe la ligi (DBF Pokal), wamefika fainali
- Europa League, wapo robo fainali
Bayer Leverkusen ambayo haijatwaa taji lolote kwa miaka 120 iliyopita inatazamiwa kuandika kutwaa rekodi ya kutwaa mataji matatu msimu huu chini ya Xabi Alonso.
Magoli ya Leverkusen kwenye mchzo wa jana yalifungwa na kiungo mshambuliaji Jnas Hoffman na mshambuliaji wao hatari Voctor Boniface ambaye ndo kwanza amerejea kutoka kwenye majeruhi.