pmbet

Lewandowski kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu.

Joyce Shedrack

May 16, 2026
Share :

Mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ataondoka Barcelona baada ya msimu huu kumalizika , Roberto amehudumu kwa misimu minne pale Catalunya.

 

Lewandowski amewaaga rasmi mashabiki wa klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku klabu yake ikithibitisha pia taarifa hizo.

FC Barcelona ruszyła z górki. Lewandowski z golem przeciwko Majorce

“Baada ya miaka minne iliyojaa changamoto na kazi kubwa, umefika wakati wa kuendelea mbele naondoka nikiwa na hisia kwamba dhamira imetimia. Misimu 4, mataji 3 ya ubingwa.

 

"Sitawasahau kamwe mashabiki kwa upendo walionionyesha tangu siku zangu za mwanzo Catalonia ni sehemu yangu duniani.

 

"Asanteni kwa kila mtu niliyepatana naye katika safari hii nzuri ya miaka minne shukrani za pekee kwa Rais Joan Laporta kwa kunipa nafasi ya kuishi kipindi cha ajabu zaidi katika maisha yangu ya soka.

 

"FC Barcelona imerudi mahali inapostahili kuwa,Visca el Barça. Visca Catalunya 💙❤️”Ameandika Lewandowski.

 

Nyota huyo amefunga jumla ya magoli 119 na ndani ya msimu hiyo minne amachukua Laliga mara 3 , Copa de la Rey mara moja na Spanish Super Cup mara 3.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet