pmbet

Liam Delap atamani kuichezea Man United badala ya Chelsea

Eric Buyanza

May 13, 2025
Share :

TalkSport imeripoti kuwa mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap angependelea zaidi kuhamia Manchester United badala ya Chelsea.

Man United na Chelsea ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 lakini Man U anapewa nafasi kubwa zaidi kuipata saini yake.

Fowadi huyo wa Ipswich amefunga mabao 12 katika mechi 35 za Ligi Kuu ya Uingereza.

Kifungu cha kuachiliwa kwa Delap kwasasa ni pauni milioni 30 kufuatia klabu hiyo kushuka daraja. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet