Libasse Gueye atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti.
Joyce Shedrack
September 11, 2026
Share :
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Libasse Gueye, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, huku akiwashinda Maxi Nzengeli wa Young Africans na Oscar Mwajanga wa Mbeya City.

Gueye ameonesha kiwango kizuri baada ya kuisaidia Simba kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi Agosti, ambapo katika Timu yake ya Simba amefunga bao moja na kuhusika katika mabao matano.





