pmbet

Licha ya kuchapwa, Fury avuna pesa nyingi kuliko Usyk

Sisti Herman

May 21, 2024
Share :

Licha ya kuchapwa na Alexander Usyk, bado Tyson Furry aliweza kuondoka na kitata kikubwa katika pambano la ngumi za kulipwa kutafuta Bingwa wa Dunia wa uzito wa juu kwenye mikanda minne tofauti lililofanyika huko Riyadh, Saudi Arabia mnamo 18 Mei 2024.

 

Kutokana na Jina lake kuwa kubwa kuliko mshindani wake, Furry katika usiku huo alikunja kiasi cha dola za kimarekani milioni 100 sawa na 70% ya pesa iliyokuwa imewekwa mezani ili miamba hiyo ipande Ulingoni.

 

Hata hivyo Alexander Usyk raia wa Ukraine hakuondoka na mkanda tu pekee bali aliweza kutoa kibindoni dola za kimarekani milioni 30 na inatarajiwa mechi ya marudiano dau kwa Usky litaongezeka kutoka na yeye kuongeza thamani kwa kumchapa Furry.

 

Usky ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kumshushia kichapo Furry tangu aanze ndondi!

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet