Licha ya ushindi kocha wa Nigeria avurugwa na Taifa Stars.
Joyce Shedrack
December 24, 2025
Share :
Kocha mkuu wa Super Eagles, Eric Chelle, amebainisha maeneo ya kuboresha timu yake inapojiandaa kwa mechi ijayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, dhidi ya Tunisia wikendi hii.
Chelle alitoa matamshi hayo kufuatia ushindi wa Nigeria dhidi ya Tanzania katika mchezo wao wa ufunguzi wa AFCON siku ya Jumanne.
Mabao kutoka kwa Semi Ajayi na Ademola Lookman yaliihakikishia Nigeria ushindi wa 2-1 dhidi ya vijana wa Miguel Ángel Gamond nchini Morocco.
Kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Tanzania kinaonyesha wazi kwamba bado kuna kazi ya kufanya,” Chelle alibainisha katika mahojiano yake baada ya mechi.
“Hasa linapokuja suala la kuua mchezo. Tunafahamu hili, na tutalifanyia kazi.”
Baada ya ushindi wao dhidi ya Tanzania, Nigeria inashika nafasi ya pili katika Kundi C, huku Tunisia ikiongoza kundi hilo baada ya ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Uganda





