Ligi ya Saudi Arabia yapangua hoja za Ronaldo.
Joyce Shedrack
February 6, 2026
Share :
Uongozi wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia (SPL) umejibu malalamiko ya nyota wa Al Nasrr Cristiano Ronaldo,wakiweka wazi kuwa hakuna mchezaji yeyote hata awe na ushawishi kiasi gani ambaye anaweza kuamua maamuzi ya nje ya klabu yake.
Taarifa hiyo imekuja kufuatia kutoridhika kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 na namna klabu yake ya Al Nassr inavyoendeshwa, hususani baada ya kutoridhishwa na ukimya wa timu hiyo katika dirisha la usajili lililopita tofauti na wapinzani wao.
"Klabu zina bodi zao, watendaji wao, na uongozi wao wa soka. Maamuzi kuhusu usajili, matumizi, na mkakati yanabaki kwa klabu hizo, ndani ya mfumo wa kifedha ulioundwa kuhakikisha uendelevu na usawa wa mashindano. Mfumo huo unatumika sawa kwa ligi nzima.
"Cristiano amekuwa sehemu ya Al Nassr tangu alipofika na amechangia ukuaji na malengo ya klabu. Kama mchezaji wa kiwango cha juu, anataka kushinda. Lakini hawezi mtu mmoja hata awe na ushawishi kiasi gani ambaye anaweza kuamua maamuzi nje ya klabu yake,Shughuli za hivi karibuni za uhamisho zinaonyesha uhuru huo wazi.Imesema taarifa ya Shirikisho hilo.





