pmbet

Ligi ya wanawake kuanza leo

Sisti Herman

November 14, 2025
Share :

 

Baada ya takribani miezi mitano kupita hatimaye pazia la Ligi ya Wanawake linafunguliwa rasmi leo zikipigwa mechi nne kwenye viwanja tofauti.

Kutokana na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ambayo ukanda wa Cecafa unawakilishwa na JKT Queens, mabingwa hao wa Bara hawataanza kulitetea taji lao hadi watakapoishia kwenye michuano ya CAF.

Msimu uliopita bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, JKT Queens alitwaa taji hilo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya kulingana pointi 47 sawa na Simba iliyomaliza katika nafasi ya pili.

Msimu huu zimeongezwa timu mbili ambazo zimefikisha idadi ya timu 12 badala ya 10 zilizoshiriki msimu uliopita. Pazia la msimu linazinduliwa na mechi nne Geita Queens ambao wamepanda Ligi Kuu msimu huu wataikaribisha Ceasiaa Queens, wakati mabingwa mara nne Simba Queens watakuwa KMC Complex kukipiga na Bilo Queens ambao pia ni wageni, huku Alliance Girls ikiivaa Fountain Gate na Ruangwa Queens ikicheza dhidi ya Yanga Princess kwenye Uwanja wa CCM Majaliwa Lindi.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet