Lil Wayne aweka rekodi ya kipekee baada ya kuachia album ya The Carter VI.
Joyce Shedrack
June 6, 2025
Share :
Rapa Lil Wayne aingia kwa mara nyingine tena kwenye Orodha ya wanamuziki wa Hip-Hop mwenye Album nyingi na ambazo huuza zaidi, na hii ni baada ya Juni 6, kuachia Album yake ya #THECARTERVI ikiwa ni katika Muendelezo wa Album zake Kwanzia 'The Carter' ya 2004.
Album hii ya 6 kutoka kwa #Weezy imechukua miaka Saba hadi kuachiwa kwake, akiwashirikisha wanamuziki kama #BigSean #KodakBlack na wengineo pamoja na watoto wake wawili
Baada ya Album hiyo ya 'The Carter VI' #LilWayne ametangaza ziara yake katika kusapoti Album hiyo kuwafikia mashabiki zake na kufanya vizuri kama ambavyo zimefanya nyinginezo, lakini pia akisheherekea Album zote za kwake alizowahi kutoa akisindikizwa kwenye ziara hiyo na wanamuziki kama #Tyga #HotBoys #NoCap na wengineo.