Linda Mwananchi yampitisha Sifuna kuchuana na Ruto 2027
Sisti Herman
September 28, 2026
Share :

Vuguvugu la kisiasa nchini Kenya Linda Mwananchi limemtangaza Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, kuwa mgmbea wake wa Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Vuguvugu hilo lilichapisha katika mtandao wake wa X kuwa lilifanya kikao na kukubaliana kumteua Sifuna kama mgombea wake kama njia ya kujibu wito wa wananchi walioshauriana nao.
Pia, viongozi wa Linda mwananchi wameelezea kuwa wamefungua milango yao wazi kwa vyama vingine vitakavyotaka kuunda muungano ili kujenga upinzani wenye nguvu katika uchaguzi wa 2027.





