Lissu agoma kesi kusikilizwa kwa njia ya mtandao
Sisti Herman
April 24, 2025
Share :
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amegoma kusikiliza kesi yake ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa njia ya mtandao (Camera) badala yake ametaka apelekwe Kisutu.
Kesi hiyo ya Lissu ambayo ina mashtaka matatu inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ambapo aliziuliza pande zote kama zipo tayari kwa ajili ya kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya Lissu kusomewa Maelezo ya Awali (Ph) ambapo wote wakajibu wapo tayari.
Kwa upande wa Lissu, Askari Magerea ambaye naye aliunganishwa kwa njia ya mtandao alisema ya kwamba Lissu amegoma baada ya kuitwa katika chumba cha video cha gereza hilo la Ukonga kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi yake, na kudai kuwa hawezi kusikiliza kwa njia hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mhini aliruhusu kuendelea na kesi bila Lissu kuwepo mtandaoni, ambapo Lissu anawakilishwa na Jopo la Mawakili takribani 28 akiwemo Peter Kibatala.