Lissu ahukumiwa kifungo cha Miaka minne jela
Sisti Herman
November 6, 2026
Share :

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka minne gerezani Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi.
Hukumu hiyo imetolewa leo, Ijumaa Novemba 6, 2026, na jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Awali, Lissu alikuwa akikabiliwa na shtaka la uhaini, lakini mahakama ilimuachia huru kwa shtaka hilo baada ya kubaini upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha nia ya kutenda kosa hilo.
Hata hivyo, mahakama ilimtia hatiani kwa kosa mbadala la uchochezi, ikieleza kuwa ushahidi uliowasilishwa ulithibitisha kosa hilo.
Adhabu hiyo ya kifungo cha miaka minne imetolewa baada ya upande wa Jamhuri kuiomba mahakama imhukumu Lissu adhabu kali, ikieleza kuwa kosa hilo lina madhara kwa amani, usalama na shughuli za kiuchumi za nchi.





