pmbet

Lissu aitaka mahakama kutenda haki.

Joyce Shedrack

July 15, 2025
Share :

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, amesema haombi huruma ya Mahakama, bali anataka taratibu za kimahakama zifuatwe ipasavyo kwa mujibu wa Katiba.

Tanzanian opposition leader Tundu Lissu defiant as he appears for treason  trial - TRT Global
Akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jujini Dar es salaam, leo Julai 15, 2025 Lissu amelalamikia kile alichokiita uchezeaji wa utaratibu wa kesi unaofanywa na Mawakili wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

"Hoja yangu ni kwamba Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama... Hii ni kinyume na wajibu wao wa kikatiba," alisema.

Mbali na kesi ya uhaini, Lissu pia anakabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uongo, ambayo kwa sasa imeahirishwa baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali maombi aliyowasilisha kupitia Masjala Ndogo ya Dar es salaam.

Katika shtaka la uhaini, Lissu anadaiwa Aprili 3, 2025, alihamasisha kuzuia Uchaguzi Mkuu ujao na kufikishwa mahakamani Aprili 10, 2025 na yuko mahabusu kwa kuwa kosa hilo halina dhamana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet