Liver hawatanii msimu huu ujue... wanautaka kweli
Sisti Herman
February 11, 2024
Share :
Klabu ya Liverpool baada ya ushindi wa jana mabao 3-1 dhidi ya Burnley imeendelea kujisimika kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, Premier League ikiwa ni masaa mawili tu baada ya Manchester City kukaa kileleni baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton.
Ushindi wa Liverpool, umeifanya ifikishe pointi 54 ikiwa ni pointi moja mbele ya Man City yenye 53, lakini ina faida ya mchezo mmoja mkononi
Mabao ya Liverpool kwenye mchezo huu yalifungwa na Diago Jota dakika ya 30, Luis Diaz dakika ya 52 na Darwin Núñez 79, huku bao pekee la Burnley likifungwa na Dara O'shea dakika 45.
Mechi nyingine imeshuhudia Tottenham Hotspur ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Brighton.
Mechi nyingine kali za ligi hiyo zitaendelea kesho wakati Man United itakapovaana na Aston Villa na Arsenal dhidi ya wababe West Ham