Liverpool hawana mpango wa kuachana na Arne Slot.
Joyce Shedrack
April 22, 2026
Share :
Kocha wa Liverpool Arne Slot anatarajiwa kuendelea na majukumu yake msimu ujao licha ya shinikizo kutokana na matokeo ya kusuasua katika mbio za ubingwa msimu huu, uongozi wa klabu hiyo unaonekana kuendelea kumuamini kwa msimu ujao hii inakuja wakati klabu hiyo ikikaribia kufuzu rasmi kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League) msimu wa 2026/27.
Liverpool iko katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Lig ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2026/27ikiwa mpaka sasa inashika nafasi ya tano baada ya kukusanya alama 55 kwenye Ligi Kuu wakiwa wamecheza mechi 33 wakifanikiwa kupata ushindi katika mechi 16, huku wakipata sare mara 7 na kukubali vichapo katika mechi 10. 
Takwimu za jumla za msimu mzima, Liverpool imecheza mechi 48 katika mashindano yote wameshinda mechi 26, wamepata sare mara 7, na wamepoteza mechi 15 kwa ujumla, wamefunga mabao 85 na kuruhusu mabao 59 dhidi yao.
Msimu huu wa 2025/26, Liverpool chini ya Arne Slot imekuwa na msimu wenye kupanda na kushuka timu hiyo imetolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na FA Cup mwezi huu wa Aprili 2026.
Unadhani uongozi wa klabu hiyo imefanya uamuzi sahihi wa kumbakiza kocha huyo?.





