pmbet

Liverpool itabaki kuwa sehemu kubwa ya maisha yangu - Jürgen Klopp

Eric Buyanza

October 7, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Ujerumani, Jürgen Klopp, amethibitisha kuwa kofia za michezo ni utambulisho na silaha kubwa ya mahaba yake kwa timu anazozifundisha na ambazo ameshazifundisha.

 

Itakumbukwa  Oktoba 4, 2026, Klopp alitikisa vyombo vya habari huku akiacha wengi wakijiuliza maswali baada ya kuonekana jukwaani akiwa amevaa kofia ya klabu yake ya zamani ya Liverpool wakati wa mchezo wa Ujerumani dhidi ya Ugiriki.

 

Akiongea baada ya mchezo huo, Klopp alisema kwa uwazi:

 

"Sasa mimi ni kocha wa Ujerumani, lakini Liverpool itabaki kuwa sehemu kubwa ya maisha yangu. Nilikaa kule kwa miaka tisa ya ushindi na machozi. Huwezi kufuta kumbukumbu hizo moyoni mwako kwa sababu tu umeanza kazi mpya" alimalizia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet