Liverpool kuruhusu watatu hawa kuondoka mwisho wa msimu
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Liverpool wameripotiwa kuwa tayari kuwaruhusu Joel Matip, Thiago Alcantara na Adrian kuondoka mwisho wa msimu, huku meneja Jurgen Klopp naye akitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu baada ya kukaa na klabu hiyo kwa miaka tisa.
Ukiweka mbali mabadiliko ya meneja yanayokuja, Liverpool pia watakuwa na mkurugenzi mpya wa michezo baada ya Jorg Schmadtke kuondoka.
Ni majuzi tu Liverpool ilithibitisha kwamba Richard Hughes ataanza kazi rasmi kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo baadae mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Hughes tayari ameamua kuwaruhusu wachezaji hao watatu kuondoka katika klabu hiyo kama wachezaji huru mwishoni mwa msimu huu.