Liverpool kuwa Mabingwa leo, Arsenal ikizuiliwa na Palace
Sisti Herman
April 23, 2025
Share :
Endapo klabu ya Arsenal leo itapoteza mchezo wao wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Crystal Palace basi klabu ya Liverpool itatawazwa rasmi kuwa Mabingwa wapya wa Ligi kuu Uingereza 2024/25.
Arsenal wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi uliobakisha mechi 5 wakiwa na alama 66, alama 13 nyuma ya Liverpool wenye alama 79.
Endapo Palace wakishinda leo basi Arsenal hatoweza kufikia alama 79 za Liverpool kwenye michezo iliyobaki.