pmbet

Liverpool Mabingwa Carabao Cup 2024

Sisti Herman

February 25, 2024
Share :

Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza imeibuka mabingwa wa kombe la ligi nchini humo maarufu kama Carabao Cup au EFL Cup baada ya kuifunga klabu ya Chelsea goli 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwa dakika 120 kwenye uwanja wa Wembley jijini London.

 

Bao la Liverpool limefungwa na nahodha wao Virjil Van Dirjk dakika za jioni 118' akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Kostantinos Tsimikas.

 

Mchezo huo umeshuhudia matukio matatu muhimu ya kushangaza yakiwemo magoli mawili yaliyokataliwa kwa msaada wa Video ya maamuzi (Video Assistant Referee VAR), la Liverpool likifungwa na Van Dijrk huku la Chelsea likifungwa na Raheem Sterling.

 

Tukio lingine ni lile la kiungo wa Chelsea Moses Caecedo kuweza kusalia uwanjani kwani kustahili kutoka kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi kiungo wa Liverpool Ryan Gravenberch

 

Liverpool inaendelea kumuaga vizuri kocha wao mkuu Jurgen Klopp ambaye wiki chache zilizopita alitikisa vyombo vya habari ulimwenguni kote baada ya kutangaza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

 

Klopp amekusanya matai 10 akiwa na Liver hadi sasa yakiwa ni pamoja na ligi ya mabingwa mara 1, Uefa Super Cup mara 1, Kombe la dunia la vilabu mara 1, Ligi kuu Uingereza mara 1, Carabao Cup mara 2, Kombe la FA mara 1 na Ngao ya jamii mara 1.

 

Pia Liverpool ndiyo timu inayoongoza kutwaa Carabao Cup mara nyingi zaidi ikifanya hivyo mara 10 ikifuatiwa nna na Manchester City iliyotwaa mara 8, Manchester United wakiwa nafasi ya tatu wakikusanya makombe 6.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet