pmbet

Liverpool na Adidas wazindua uzi wa tatu msimu wa 2026/27

Eric Buyanza

August 28, 2026
Share :

Klabu ya Liverpool imezindua rasmi jezi yake ya tatu (Third Kit) kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano wa 2026/2027. Uzinduzi huu umefanyika Alhamisi ya tarehe 27 Agosti, 2026, huku ukipokelewa kwa hisia chanya na mashabiki duniani kote. Hii inakuwa jezi ya tatu kukamilisha mkusanyiko wa uzi wa klabu hiyo baada ya ule wa nyumbani na ugenini.

 

Jezi hiyo iliyotengenezwa na kampuni kubwa ya vifaa vya michezo ya Adidas, inakuja na muonekano wa kipekee unaochanganya mitindo ya kisasa na historia ya klabu:

Ina urembo wa rangi ya damu ya mzee (maroon) inayowakilisha bendera na mabango yanayopepea kwenye jukwaa maarufu la 'Kop' pale Anfield.

Pia nembo ya klabu ya 'Liver Bird', chapa ya Adidas, na wadhamini Standard Chartered zote zimewekwa kwa rangi ya fedha inayong'aa (metallic silver).


Uongozi wa Liverpool umeeleza kuwa jezi hii si tu kwa ajili ya uwanjani, bali imeundwa pia kama vazi la mitindo ambalo mashabiki wanaweza kulivaa kokote.

Uzinduzi huo umeambatana pia na ufunguzi wa duka jipya la mtandaoni la klabu hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa kwa mashabiki wa kimataifa.Jezi hii inatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni kwenye michezo ya ugenini, hasa ile ya mashindano ya kombe la Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet