Liverpool, United watoshana nguvu PL
Sisti Herman
December 17, 2023
Share :
Mchezo wa ligi kuu Uingereza uliowakutanisha majogoo, Liverpool waliowakaribisha mahasimu wao wa Uingereza Manchester United kwenye dimba la Anfield umemalizika kwa sare tasa ya 0-0.
Baada ya matokeo hayo sasa Liverpool anashuka hadi nafasi ya pili huku Man Utd ikisalia nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi hadi kufikia raundi ya 17.