Liverpool vinara UEFA Real Madrid hali tete.
Joyce Shedrack
November 28, 2024
Share :
Baada ya ushindi wa goli 2-0 walioupata Liverpool usiku wa jana katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi Real Madrid klabu ya Liverpool imekusanya alama tatu zilizowafanya kuongoza msimamo wa mashindano hayo huku Madrid ikiwa nafasi ya 24 kwenye msimamo huo.
Bingwa mtetezi wa Mashindano hayo Real Madrid ameanza vibaya msimu huu akifungwa mechi tatu na kushinda michezo miwli pekee na kukusanya jumla ya alama 6 wakati Liverpool akishinda michezo yote mitano na kujikita nafasi ya kwanza akiwa na jumla ya alama 15.
Mashindano hayo ambayo yanachezwa kupitia mfumo mpya baada ya kubadilishwa kutoka ule wa awali timu 36 zinashiriki kwa mfumo wa ligi kila timu ikicheza mechi nane nyumbani na ugenini na timu nane za juu kwenye msimamo wa ligi zitafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora huku timu zilizoshika nafasi ya 9 hadi ya 24 zikicheza hatua ya mtoano na timu zitakazomaliza nafasi 25 hadi ya 36 zitatupwa nje ya mashindano hayo moja kwa moja.
Real Madrid imebakiza mechi tatu za kuamua hatma yao kwenye mashindano hayo huku mchezo mmoja pekee ndio watakaokipiga Santiago Bernabeu kwenye uwanja wao wa nyumbani3 dhidi ya RB Salzburg na michezo miwili ugenini dhidi ya Atalanta na Stade Brest.