Liverpool waambiwa watoe pauni milioni 100 kama wanamtaka Jamal Musiala
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Bayern Munich wameripotiwa kuweka bei ya pauni milioni 100 kwa Jamal Musiala anayehusishwa na Liverpool kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Musiala amejihakikishia namba kwenye kikosi cha Bavarians pale Allianz Arena, akiwa ameshacheza mechi 155 na kufunga mabao 41.
Klabu ya Liverpool imeonekana kuwa na nia ya dhati ya kutaka huduma za chipukizi huyo mwenye asili ya Uingereza.