Liverpool wachapwa Anfield, mashabiki waondoka uwanjani
Sisti Herman
April 12, 2024
Share :
Ikiwa ni siku chache tu tangu kutoka sare na vibonde wa "Top 6" ya ligi kuu Uingereza Manchester United, klabu ya Liverpool jana imeendeleza mwendo wa kusuasua kusaka mataji inayoshindania mara baada ya kufungwa magoli 3-0 na Klabu ya Atlanta ya Italia kwenye mchezo wa robo fainali ya Europa League kwenye dimba lao la nyumbani, Anfield.
Atlanta imeweka rekodi ya kushinda Anfield huku pia ikiwa timu pekee kushinda kwenye dimba hilo kwenye miezi 14 iliyopita.
Magoli ya Atlanta kwenye mchezo huo yalifungwa na Gianluca Scamacca aliyetupia mawili na Mario Pasalic.
Liverpool wana mlima mrefu wa kupanda ilikuweza kuvuka hatua hii kwenye mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa Italia.