Liverpool wahusishwa na mshambuliaji wa Leeds, Summerville
Eric Buyanza
May 28, 2024
Share :
Liverpool wanaweza kumsajili winga wa Leeds, Crysencio Summerville badala ya Gordon wa Newcastle.
Msimu mzuri aliokuwa nao Summerville unamfanya kuwa mchezaji anayesakwa na klabu nyingi kubwa za ulaya.
Siku kadhaa zilizopita, Liverpool walihusishwa na usajili wa winga wa Newcastle United, Anthony Gordon, kabla hawajabadii maamuzi yao na kuhamishia nguvu kwa fowadi wa Leeds, Crysencio Summerville.