Liverpool wapata mrithi wa Klopp, anatoka Uholanzi
Sisti Herman
April 27, 2024
Share :
Klabu ya Liverpool ya Uingereza imefikia makubaliano na Feyenoord ya ligi kuu Uholanzi juu ya kumchukua kocha wao Mkuu Arne Slot kwa ajili ya kuwa kocha mkuu klabuni hapo akichukua mikoba ya Jürgen Klopp ambaye ataondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu.
Slot (45) anatarajiwa kuanza kazi kama kocha mkuu ya Liverpool kuanzia msimu ujao baada ya Feyenoord kuafikiana na Liverpool juu ya fidia ya kumwachia kocha huyo raia wa Uholanzi.
Je ni mrithi sahihi wa Klopp?