Liverpool yahamishia majeshi kwa Ekitike baada ya kumkosa Isack.
Joyce Shedrack
July 17, 2025
Share :
Klabu ya Liverpool ipo kwenye hatua nzuri ya kunasa saini ya mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt raia wa Ufaransa Hugo Ekitike kama chaguo la pili baada ya kumkosa Alexander Isak kutoka Newcastle United .
Mabingwa hao wa Uingereza wanaripotiwa kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu Nchini Ujerumani pamoja na kambi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kujadili masharti ya mwisho ili kufikia makubaliano ya kuitumikia Liverpool msimu ujao.
Liverpool wameamua kumgeukia Ekitike ambaye msimu uliopita amefunga magoli 15 na kutoa pasi 8 za magoli baada ya kumkosa Isak ambaye klabu yake imegoma kumuuza.