Liverpool yaichomolea Juventus kwa Alisson Berker
Sisti Herman
May 29, 2026
Share :

Liverpool 'imeifunguia vioo' Juventus iliyoonyesha nia ya kutaka saini ya kipa Alisson Berker.
Juventus walikuwa wamempa Alisson kandarasi ndefu zaidi kwa mradi wa miaka mitatu, lakini Liverpool walimwambia Alisson wanamtegemea.
Mawasiliano rasmi pia yaliyofanywa kwa Alisson na kambi yake wakati Mamadashvili akitoka kwa mkopo yanaweza kuzingatiwa msimu huu wa joto.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Alisson anabaki Liverpool isipokuwa kuwe na mabadiliko au msimamo wake ubadilike.





