Liverpool yajitoa kuwania saini ya Alonso
Sisti Herman
March 29, 2024
Share :
Klabu ya Liverpool imejitoa rasmi kwenye mbio za kuwania saini ya kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ambaye pia alikuwa mchezaji wao wa zamani wakiamini kuwa ana uwezekno mkubwa kuendelea kusalia Leverkusen.
Baada ya Liver kujitoa kwenye mbio hizo nafasi kubwa kwasasa ni Alonso kusalia kwenye klabu yake huku Bayern Munich na Real Madrid wakendelea kupigana vikumbo kuhitaji saini yake.
Ikumbukwe kuwa Xabi anaiongoza Bayern Leverkusen hadi sasa na ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa mchezo hata mmoja kwenye mashindano yote huku wakipewa chapuo kushinda mataji kama Bundesliga, DFP Pokal na Europa League.