Liverpool yaondolewa Ulaya
Sisti Herman
April 19, 2024
Share :
Jinamizi la kuagwa vibaya kwa kocha Jurgen Klopp aliyetangaza kuondoka mwishoni mwa msimu huu limeendelea kuikumba klabu ya Liverpool baada ya jana kuondoshwa kwenye michuano ya Europa League licha ya kushinda 1-0 ugenini Atlanta.
Liverpool wameondoshwa kwa jumla ya mabao kwenye mechi za mikondo miwili (aggregate) kwani ilitoka kupoteza Anfield wiki iliyopita.