Lobota Bola kutua Yanga au Singida?
Eric Buyanza
December 13, 2023
Share :
Taarifa zikufikie kuwa kwenye dirisha dogo la usajili, winga hatari kutokea nchini Congo Manu Lobota Bola wa klabu ya FC Lupopo anakuja kucheza Tanzania.
Kupitia maswali aliyoulizwa na mwandishi wetu kupitika ukurasa wake wa Instagram Lobota alikiri kuja kucheza Tanzania lakini akagoma kuitaja timu anayokuja kuchezea.
Hata hivyo tetesi zinasema huenda mchezaji huyo anakuja kuichezea Yanga au Singida Fountain Gate.
Bola ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Lobota Bola ni moja ya mawinga bora waliobaki nchini Congo kwasasa.