pmbet

Lookman alivyotumia hasira za AFCON kuwapa Atlanta taji la Europa

Sisti Herman

May 23, 2024
Share :

Hat-trick Hero...! Unaweza kumwita hivyo Ademola Lookman, kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Nigeria ambayo ilikosa taji la AFCON 2023 kwenye fainali dhidi ya Ivory Coast ambaye jana alimaliza hasira zake zote za AFCON kwenye fainali ya Europa League dhidi ya Bayer Levekursen ya kocha kijana mtanashati Xabi Alonso.

Kwanini Lookman? kiungo huyo ndiyo aliyefunga mabao yote matatu ya ushindi kwenye mchezo huo wa fainali ambapo Levekursen walifungwa 3-0 kwenye dimba la Aviva jijini Dublin nchini Ireland.

Hizi ni takwimu za kiungo huyo mchezo huo;

- Dakika alizocheza 90
- Mashuti yaliyolenga lango 3
- Magoli 3

Lookman alifunga mabao yake dakika ya 12, 26 na 75 na kuwapa Atlanta taji lao la kwanza Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet