Luis Enrique alivyotumia Goalkick za Safonov kuficha ubora wa Olise
Sisti Herman
May 9, 2026
Share :

Utangulizi
Bayern Munich waliwakaribisha Paris Saint-Germain katika Uwanja wa Allianz Arena kwa mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya UEFA Champions League, Pambano hilo liliisha kwa sare ya 1-1, jambo ambalo lilimaanisha kuwa PSG walitoka kwa jumla ya mabao 6-5.
Ousmane Dembélé alifunga bao la mapema na kuwapa makali Les Parisiens, huku Bayern ikilazimika kuwinda kwa muda wote uliosalia wa mchezo; hatimaye walirudisha moja nyuma kupitia kwa Harry Kane wakati wa muda wa nyongeza, ambao ulionekana kuchelewa sana kwao kupata mwingine wa kulazimisha muda wa ziada.
Mchezo huo wa mkondo wa pili ulikuwa tofauti sana na wa kwanza; PSG walichagua mbinu ya kisayansi zaidi, ambayo iliwasaidia kuwaweka nje wapinzani wao kwa sehemu kubwa.
Vikosi
Hebu tuangalie jinsi Vincent Kompany na Luis Enrique walivyopanga vikosi vyao.
Bayern walicheza katika mfumo wa 4-2-3-1.
Nahodha Manuel Neuer alianza goli.
Wachezaji wanne nyuma walikuwa Konrad Laimer (beki wa kulia), Dayot Upamecano (beki wa kati wa kulia), Jonathan Tah (beki wa kati wa kushoto), na Josip Stanišić (beki wa kushoto).
Upamecano, Tah, na Stanišić walibadilishwa na Lennart Karl (85’), Kim Min-jae (68’), na Alphonso Davies (67’), mtawalia.
Joshua Kimmich na Aleksandar Pavlović walicheza kama pivoti mbili.
Michael Olise (kulia) na Luis Díaz (kushoto) walikuwa mawinga wawili, huku Jamal Musiala akiwa kiungo mkabaji.
Nicolas Jackson alichukua nafasi ya mwisho baada ya dakika 79.
Harry Kane alicheza kama mshambuliaji.
PSG walicheza katika mfumo wa 4-3-3.
Matvey Safonov alianza kati ya vijiti.
Wachezaji wanne nyuma walikuwa Warren Zaïre-Emery (beki wa kulia), nahodha Marquinhos (beki wa kati wa kulia), Willian Pacho (beki wa kati wa kushoto), na Nuno Mendes (beki wa kushoto).
Bao la pili lilimwachia nafasi Senny Mayulu dakika ya 85.
Vitinha, João Neves, na Fabian Ruiz walikuwa safu ya kiungo watatu.
Ruiz alibadilishwa na Lucas Beraldo (76’).
Watatu wa mbele walikuwa Désiré Doué (winga wa kulia), Ousmane Dembélé (mshambuliaji), na Khvicha Kvaratskhelia (winga wa kushoto).
Doué na Dembélé walichukua nafasi kwa Lucas Hernández (76’) na Bradley Barcola (65’), mtawalia.
Ubora wa Mbinu za PSG chini ya kocha Luis Enrique
1. Mkakati wa kutumia GoalKick za Safonov
Mara zote PSG wakiwa na mpira ujenzi wao wa shambulizi kutoka nyuma ulianza kwa mipira mirefu ya juu ambayo mingi kati ya hiyo ilitoka nje au kuwa ya kugombania ambapo kati ya pasi ndefu 33 alizopiga, ni pasi 7 ndizo zilizofika kwa wachezaji wa PSG

Kwa soka la kisasa unaweza kudhani kuwa ilikuwa ni makosa ya kujirudia lakini kumbe ulikuwa mkakati binafsi wa kocha Luis Enrique kwani alifanya tathmini nzuri kwa namna Bayern wanacheza na kutengeneza mpango huo uliokuja na suluhisho la;
1. Kwa namna Bayern wanavyozuia kwa shinikizo kubwa (High Pressure difensive style) langoni mwa wapinzani wao ni ngumu kuanza kujenga shambulizi kuanzia nyuma kwa pasi fupi na kuweza kutoka kwenye shinikizo lao
2. Mpango wa kutumia mipira mirefu ni rahisi kuficha ubora wa kiufundi wa wachezaji wabunifu wa Bayern kama Michael Olise kwani, Safonov alipiga mipira mirefu mingi mbele, kati ya hiyo mingi ilitoka na mingine ikawa ya kugombania, hapo ndipo mkakati wa PSG ulipokuwa
Kwenye mipira ya iliyotoka PSG walihakikisha wanahamia upande huo wengi ili kuwa kwa idadi kubwa na kuwanyima wachezaji wabunifu wa Bayern kama Olise muda na nafasi ya kuwa na mpira (Under Pressure) kisha kuzuia kwa shinikizo kubwa kuwapora mipira na kujibu shambulizi (Forcing Turnovers)

Kwenye mipira iliyobaki ya kugombania pia PSG walikuwa na mkakati wa kuhakikisha wanashinda mipira ya juu na ya chini (Duels) ili kuweza kushinda na kujibu shambulizi karibu zaidi na goli la Bayern.
2. Uzuiaji bora wa PSG ( Difensive Pressing & Blocks)
Kila Bayern walipokuwa na mpira kwenye theluthi yeyote ya uwanja PSG walihakikisha wanazuia kwa shinikizo kubwa, wengi nyuma ya mpira na wakiwa wamejipanga kwenye muundo mzuri wa kuzuia njia za Bayern kuweza kuwafikia kirahisi;
Theluthi ya mbele (High Press)
PSG walizuia na muundo wa 4-3-3 ambapo mbele walikuwa na Dembele, Khvira na Doue dhidi ya wachezaji wa Bayern walikuwa wakijenga shambulizi na muundo wa 3-4-3-1

Theluthi ya kati (Mid Press)
Mpira ukitoka kwenye theluthi ya mbele na kuanza kufika kwa viungo, PSG walizuia na staili ya mtu kwa mtu (Man Marking) kwa shinikizo kubwa sana hasa kwa viungo na wachezaji wa nyuma wa Bayern ili kuwanyima muda na nafasi ya kuwa wabunifu na kulazimika kufanya makosa.

Theluthi ya nyuma (Difensive Block)
Kwenye theluthi yao ya mwisho PSG walizuia wengi nyuma ya mpira kwa shinikizo la chini na kuzuia njia za Bayern kuweza kufika langoni mwao kirahisi, njia za kati na za pembeni

Nyakati nyingi walizuia mpira usiweze kupita katikati kwa Kimmich na Pavlovic kucheza na Musiala na Harry Kane kisha wakalazimisha Bayern kupita pembeni kwa Olise na Diaz na huko wakaweka mkakati wa kuzuia kwa idadi kubwa

Mpira ukiwa kwa Diaz beki wa kulia anamfuata kisha winga wake, mara nyingi Doue/ Dembele anaziba njia ya Diaz kukokota mpira kuja ndani wakimlazimisha acheze nje kwani huwa na madhara kidgo kutengeneza nafasi na kufunga

Mpira ukiwa kwa Olise vivyo hivyo, Nuno Mendez humfuata na kumlazimisha akokote kuelekea nje, huku beki wa kati akiziba nafasi nyuma yake na kiungo wa kati Fabien Ruiz akiziba njia ya Olise kuingia na mpira ndani.
Mwisho, Mbinu hizi zisaidia PSG kutawala mchezo, wakiwa na mpira na hata bila mpira kisha wakaweza kuvuka na kuingia fainali ambapo watacheza dhidi ya Arsenal huko Budapest.





