pmbet

Lulu aandika ujumbe mzito kwa Majizzo wakitimiza miaka 5 ya ndoa yao.

Joyce Shedrack

February 16, 2026
Share :

Staa wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu Lulu pamoja na mume wake mfanyabiashara maarufu ambaye ni mmiliki wa EFM na TVE Francis Ciza  wametimiza miaka mitano ya ndoa yao tangu walipofunga pingu za maisha february 16,2025.

Majizo ataja sababu ya kufunga ndoa kimyakimya na Lulu | Mwanaspoti

Katika kusherekea kumbukumbu yao ya miaka 5 Lulu ameandika ujumbe mzito  kwa mume wake huku akiweka waz mahaba yao hayapimiki.

“ Kwa NEEMA ya MUNGU tukaone mitano tena na zaidi 🙏"

"Ba’Mpenzi,Ba’mtu,Winga wa moyo wangu umepita bila kupingwa Baba 🤝😁 Uongozi wako hauna vipengele bwana…Japo WACHAGA na WAHAYA walinibadilisha kwa kreti za bia na mikungu ya ndizi 😭 ila hujawaangusha kiongozi…!

“Ahsante kwa KUNIPENDA,KUNILEA na KUNITUNZA mumewangu (mana nazidi kuwa mdogo mdogo kama mandonga ujue😂)”

“Sasa kuna mchongo nausikilizia,mambo yakienda sawa…nakuchapa na PRIVATE JET 🛩️ mtoto wa Ma’mkwe…si unanijua kuhusu malavidavi hii level chafu bebi 👌”

“Happy 5th Anniversary Mumewangu❤️kama MOYO ni nchi nakukabidhi kwa muhula mwingine mwaego 🤝😁inaninogea sana kufanya haya maisha na wewe MKUU 😘”

“Baada ya kusema yote hayo sasa nihitimishe kwa kusema…fanya jambo LINE yangu😂😂😂NIPULIZIE baba…ile meseji ya IMETHIBITISHWA inishukie kwa ngurumo kubwa ikikupendeza 🙏 Nakupentaaaa😂”Ameandika Lulu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet