Lulu Diva afunguka ugomvi wake na Wema Sepetu amtaja Whozu.
Joyce Shedrack
January 10, 2026
Share :
Licha ya Wema Sepetu na Lulu Diva urafiki wao Mara kadhaa huingia kwenye maugomvi Kama ilivyo kawaida kwa marafiki wengine kike, ila kwa sasa hivi imekuwa tofauti kidogo baada ya Lulu Diva kuandika ujumbe mzito kwenye Mtandao akielezea mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakimuudhi ikiwemo jina lake kuchafuliwa kuwa anatoka kimahusiano na Whozu ambae ni Mpenzi wa Rafiki yake.
Kiufupi Lulu Diva ameliweka sawa jambo Hilo na kusema wazi kuwa Whozu ni Rafiki yake tu na ni wa Muda Mrefu tangu kipindi ambacho Whozu na Wema hawajaingia kwenye mahusiano akisema kuwa yeye Kutokuwa sawa na Wema haimaanishi awe na uadui na Whozu.
Lulu Diva amemalizia kwa kusema kuwa suala la yeye kugombana na aliyekuwa Rafiki yake (Wema) haoni haja ya yeye kuweka mitandaoni ila chanzo cha ugomvi wao sio yeye kutoka kimahusiano na Whozu.





