pmbet

Lupita Nyong'o kwenye penzi jipya!

Eric Buyanza

December 6, 2023
Share :

Ikiwa ni wiki moja tu tangu mahusiano yake na mpenzi wake kuvunjika, msanii wa filamu na mshindi wa tuzo za Oscar kutoka pande za U.S.A mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong'o amenaswa na mapaparazi akivinjari kimahaba na mwigizaji raia wa Canada Joshua Jackson kwenye mgahawa mmoja jijini Los Angeles.
 

Joshua na Lupita wamejuana kwa muda mrefu, lakini walionekana wakiwa karibu zaidi  kwenye tamasha la Janelle Monae hivi karibuni, kitendo kinachoelezwa kuwa chanzo cha kuparaganyika kwa penzi lake na Sal Masekela.
 

Kwa upande wa Joshua haya yanakuja ikiwa ni wiki kadhaa tu tangu ndoa yake na mwanamitindo Jodie Turner-Smith iliyodumu kwa miaka minne kuvunjika. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet