Lusajo aaga rasmi Namungo
Sisti Herman
December 25, 2023
Share :
Nahodha na mchezaji mwandamizi wa klabu ya Namungo ambaye pia ni mshambulaiji wao bora tangu wapande ligi kuu Reliants Lusajo ameaga rasmi kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
“Napenda Kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Namungo na benchi la ufundi bila kusahau washabiki wote wa timu ya namungo kwa kipindi chote tulichokua pamoja ni Muda wangu sasa wa kuangalia changamoto sehemu nyingine nipende kuwatakia kila la kheri katika msimu huu wa ligi” aliandika mshambuliaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Lusajo ambaye ni mmoja kati wachezaji wasomi zaidi kwenye ligi kuu anategemewa kujiunga namoja kati ya timu za ligi kuu pia ikumbukwe aliwahi kuitumikia Yanga kabla ya kwenda kuendelea na masomo kwenye chuo cha ushirika Moshi.