Lusajo ajiunga rasmi na Mashujaa
Sisti Herman
January 11, 2024
Share :
Aliyekuwa mchezaji mwandamizi na nahodha wa klabu ya Namungo FC ya mkoani Lindi Reliants Lusajo amejiunga na kutambulishwa rasmi na klabu ya Mashujaa FC ya Kigoma, zote zikishiriki ligi kuu Tanzania bara.
Lusajo ambaye aliaga Namungo wiki kadhaa zilizopita alihusishwa pia kujiunga na Azam Fc kabla ya matajiri hao wa Dar es salaam kumtambulisha mshambuliaji raia wa Colombia Franklin Navarro.