pmbet

Lwandamina amvulia kofia Straika mpya Simba

Sisti Herman

January 19, 2024
Share :

Siku chache tangu Simba imnase na kumtangaza mshambuliaji mpya, Freddy Kouablan kutoka Green Eagles ya Zambia, kocha wa zamani wa Yanga na Azam FC, George Lwandamina amevunja ukimya na kusema Wekundu wa Msimbazi wamelamba dume kwa kumpata straika huyo.

Freddy, raia wa Ivory Coast ametua Simba kwa mkataba wa miaka miwili, akiwa na rekodi nzuri katika Ligi Kuu ya Zambia baada ya kuhama Green Eagles akiwa ameifungia mabao 14 na kuasisti mara nne katika mechi 16, jambo linalowapa matumaini mapya wapenzi wa wekundu hao.

Lwandamina alisema, “Mshambuliaji mzuri Simba imepata mtu, hakuna mchezaji wa namna yake tangu msimu ulipoanza atawapa vitu vingi sana na ataziba mapengo mengi kwani ana nguvu na akili ya kuwatoka mabeki, pia kufunga na kujitenga ili aweze kutengeneza nafasi ya bao.“

“Hata hivyo, kufanya kwake vizuri kwenye Ligi ya Tanzania itategemeana na yeye kuzoea mazingira na ubora wa timu lakini pia falsafa ya kocha kama hivyo vikiwa sawa basi msimu utaisha vizuri sana kwa Simba.”

Kwa sheria za CAF mshambuliaji yuko huru kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, Februari 23 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet