M23 waiteka Lumbishi mji maarufu kwa uchimbaji wa madini
Eric Buyanza
January 20, 2025
Share :
Wapiganaji wa kundi la waasi linaoungwa mkono na Rwanda la M23, wamechukua udhibiti wa eneo muhimu la uchimbaji madini nchini Kongo.
Wakazi wameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba kundi hilo lenye silaha lilichukua udhibiti wa mji wa Lumbishi, eneo lenye utajiri wa madini katika mkoa wa Kivu Kusini juzi Jumamosi, kabla ya kuelekea Numbi na Shanje, maeneo mengine mawili katika jimbo jirani la Kalehe.