pmbet

M23 yasema imeanza kuondoa wanajeshi wake katika mji wa Uvira

Eric Buyanza

December 18, 2025
Share :

Waasi wa M23 jana Jumatano jioni wamedai kuwa wameanza kuondoka kwenye mji waliokuwa wakiushikilia wa Uvira uliopo mashariki mwa DR Congo.

Bertrand Bisimwa, kiongozi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda ameliambia shirika la habari la AP kwa njia ya simu kwamba zoezi la kuondoka kwenye mji huo litakamilika asubuhi ya leo.

Pia vyanzo vya ndani na wawakilishi wa mashirika ya kiraia wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi wa M23 wameanza kuondoka katika jiji hilo, wakielekea kaskazini.

"Ninapozungumza nanyi, tunaona magari ya kijeshi ya M23 yakiondoka katika jiji hilo yakielekea kaskazini, labda kuelekea Luvungi," mkazi mmoja amesema kwa simu.

"Niliwaona katika safu, wakiwa na mifuko yao ya kijeshi na silaha, wakielekea barabara kuu nambari 5," barabara kuu ya eneo hilo, ambayo inapita kando ya mpaka wa Burundi kuvuka Bonde la Ruzizi, amesema mkazi mwingine.

M23 walichukua udhibiti wa mji huo wiki iliyopita kufuatia mashambulizi iliyoyaanzisha mapema mwezi huu licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani na kusainiwa na marais wa Kongo na Rwanda.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet