Ma Pro waliopishana dirishani Azam
Sisti Herman
January 26, 2024
Share :
Klabu ya Azam FC kupitia idara yao ya habari imetoa ripoti fupi ya uhamisho na usajili kwa wachezaji wa kimataifa kwenye dirisha dogo la usajili liliotamatika Januari 15 huku wakitoa sababu mbalimbali zilizotumika kufanya usajili na uhamisho.
Wachezaji wa kimataifa walioondolewa kwenye usajili wa Azam kwenye dirisha dogo lililopita
1. Idris Mbombo (Ameondoka)
2. Idrissu Abdilahi (Majeraha ya muda mrefu)
3. Ali Ahmada (Majeraha ya muda mrefu)
Wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa kwenye usajili wa Azam dirisha dogo lililopita
1. Franklin Navarro (Colombia)
2. Mohamed Mustafa (Sudan)
3. Yeison Fuentes (Colombia)